Tuesday, 24 March 2015

BAADA YA MVUA KALI KUANZA KUNYESHA DAR ES SALAAM MAZINGIRA SASA YAKO HIVI

Hizi ni picha mbali mbali zikionyesha mazingira ya Dar es salaam baada ya mvua kali kuanza kunyesha mwezi huu wa tatu ambapo majuzi baada ya mvua kushinda zinanyesha kunavijana wawili maeneo ya kimara bonyokwa walikuwa wakitoa msaada wa kusukuma gari lilokwama kwenye matope lakini ikawa ni bahati mbaya kwao baada ya gari hiyo kugonga nguzo na kuwadondokea na kupoteza maisha hapo hapo.

Pia kwanupande wa usafiri umekuwa ni shida sana kwa wananchi ambao kila baada ya kazi ni  lazima wajirudishe majumbani kwao lakini imekuwa ni shida kwa wakazi wa mbagala, buguruni,vingunguti,kiwalani na kimara baada ya barabara kujaa maji na magari kushindwa kupita kwa urahisi kama hapo awali.

Pia ni kama miezi miwili sasa tangu nitengeneze makala ya kituo kipya cha usafirishaji wa abiria ambacho kilikuwa ubungo na baadae wakahamishia maeneo ya sinza mgabe na kukipa jina la simu2000 kutokana na namba ya kiwanja hicho. Kulikuwepo na maoni tofauti tofauti kwa wananchi mbalimbali kutokana na miundo mbinu ya barabara inayotumika na magari ama daladala ambazo huingia humo ndani ya kituo hicho haina kiwango cha lami na wakati wa jua huwa kunavumbi kubwa sana ambalo kiusalama si zuri hasa kwa abiria na wakaazi wa eneo hilo kijumla.

Na pia wakati wa mvua kuna kuwa na madimbwi ya maji na matobe ambayo huingia ndani ya kituo hicho na kuziba mitaro ambayo hutumika kutoa maji wakati wa mvua kunyesha kitu ambacho sasa kimeanza kutokea baada ya mvua hizi za mwezi wa tatu kuelekea mwezi wa nne kuanza. sasa mazingira ya kituo hicho yameanza kubadirika baada ya matobe kutoka barabara ya vumbi kuanza kuzagaa ndani ya kituo na madimbwi ya maji hapa na pale kuonekana yamejaa.

Pia kwa wakazi wa vingunguti kwao imekuwa ni shida kubwa sana kwao kwa kuanza msimu huu wa mvua za masika baada ya mtaro mkuu wa kutolea maji taka na maji ya mvua kuziba. Mtaro huo uliziba na wananchi bila kugundua kitu, bali waligundua baada ya kuona maji yanazidi kujaa kupita kiasi cha kawaida ambacho kimezoeleka siku zote.
Mtaro huo uliziba nyakati za usiku ambapo kwa wananchi wasio waaminifu wakaanza kuzibua maji taka na kuacha yazolewe na mkondo wa maji ambao ulikuwa hautembei.
Baadae ikawa ni shida kubwa sana kwao kwa maji kutanda na kuzagaa kila mahali ndipo wakagundua kuwa mkondo huo hautembei. Baada ya kugundua hilo mamlaka ya serikali za mtaa waliamulu kuvunja baadhi ya nyumba takribani tatu ili kutafta ni wapi mkondo ulipoziba kitendo ambacho kilikuwa nikigumu sana kwa baadhi ya wananchi kukubali kuharibiwa makaazi yao na ni wakati wa mvua kama hizi ambazo zinanyesha bila kukoma kwa siku nzima mfururizo.

Hii inakatisha tamaa sana baada ya kuona viongozi wetu wanajisahau kutengeneza miundo mbinu mpaka wakati wa mvua na wananchi wanaaanza kutaabika kwa kusumbuka kimakazi na miundombinu ya usafiri inakuwa shida kwao, wanachi tofauti wa makazi  ya jiji la dar es salaam wamekuwa wakilalamika miaka nenda mpaka sasa nahisi wamechoka na kuamua kubaki kimya na kulidhika na hali halisi ya maisha yao kuendelea kwa mtindo huo huo.

Serikali inaombwa kutoa ushirikiano na kuisaidia jamii kwa kurekebisha miundo mbinu ya usafiri ili kuboresha maendeleo ya jamii ambayo inaunda serikali yao wenyewe. Pia wanajamii wanapaswa kuwa wanawakumbusha viongozi wao kila mara na kuweka vikao vya jumuia ilikuangalia maendeleo yao na badiliko kwa msimu wa miezi sita na kuweka malengo kubolesha mazingira yanayowazunguka kwa kusoma nyakati za misimu ya mwaka kama wakati wa mvua na wakati wa jua.

Saturday, 21 March 2015

Samsung Galaxy S3 Neo

SIMU INAUZWA KWA BEI POA KABISA IMENUNULIWA KUTOKA UJERUMANI BADO MPYA KABISA ANGALIA SPECS ZAKE HAPO NA UNIPIGIE SIMU NIKUPE BEI;
0784644233/07555488169/0719357108

Available as:
Samsung SIII Neo+ I9300I
Samsung GT-I9300RWI with no NFC connectivity
NETWORK Technology
GSM / HSPA
LAUNCH Announced 2014, April
Status Available. Released 2014, April
BODY Dimensions 136.6 x 70.8 x 8.6 mm (5.38 x 2.79 x 0.34 in)
Weight 132 g (4.66 oz)
SIM Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by)
DISPLAY Type Super AMOLED capacitive touchscreen, 16M colors
Size 4.8 inches (~65.7% screen-to-body ratio)
Resolution 720 x 1280 pixels (~306 ppi pixel density)
Multitouch Yes
PLATFORM OS Android OS, v4.3 (Jelly Bean), upgradable to v4.4.4 (KitKat)
Chipset Qualcomm MSM8226 Snapdragon 400
CPU Quad-core 1.2 or 1.4 GHz Cortex-A7
GPU Adreno 305
MEMORY Card slot microSD, up to 64 GB
Internal 16 GB, 1.5 GB RAM
CAMERA Primary 8 MP, 3264 x 2448 pixels, autofocus, LED flash
Features Simultaneous HD video and image recording, geo-tagging, touch focus, face/smile detection
Video 1080p@30fps
Secondary 1.9 MP, 720p@30fps
SOUND Alert types Vibration; MP3, WAV ringtones
Loudspeaker Yes
3.5mm jack Yes
COMMS WLAN Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, Wi-Fi Direct, hotspot
Bluetooth v4.0, A2DP, EDR, apt-X
GPS Yes, with A-GPS, GLONASS
NFC Yes
Radio Stereo FM radio with RDS
USB microUSB v2.0
FEATURES Sensors Accelerometer, gyro, proximity, compass
Messaging SMS(threaded view), MMS, Email, Push Mail, IM
Browser HTML
Java Yes, via Java MIDP emulator
  - S-Voice natural language commands and dictation
- Smart Stay eye tracking
- Active noise cancellation with dedicated mic
- MP4/WMV/H.264 player
- MP3/WAV/eAAC+/FLAC player
- Photo/video editor
- Document viewer
BATTERY   Li-Ion 2100 mAh battery
Stand-by Up to 330 h (2G) / Up to 340 h (3G)
Talk time Up to 14 h (3G)
Music play Up to 57 h

Monday, 16 March 2015

Rose ndauka aungana  na sure herbal clinic kupinga na kukomesha kabisa mauaji ya albino yanayoendelea hapa nchini Tanzania. Sure herbal clinic ambayo inafanya vizuri katika matibabu ya tiba asilia na matunda sasa itabadili jina la clinic hiyo na kuitwa Sigwa herbal clinic ambapo tabibu simon rusigwa ametoa angalizo kwa uma na jamii kwa ujumla kwamba kubadilika kwa jina hakuchangii kubadilika kwa kitu chochote kwa huduma za matibabu yao.

MAZINGIRA YETU

Hapa ninjiji Dar es salaam maeneo ya Kimara mwisho ambapo ipo wilaya ya Temeke, maeneo haya hamna mpangilio mzuri wa usafi hasa kando kando ya barabara na ukiingia ndaninpia katika makazi ya watu kuna majalala ambayo ni uchafu unaonuka na kutoa harufu kali ambayo kiafya si nzuri.

HATIMAYE MVUA ZAANZA KUNYESHA DAR ES SALAAM

Baada ya muda wa kama miezi mitano kutoka mvua za vuli zilipo anza kunyesha hapa jijini Dar es salaam kisha zikasita kwa muda mrefu sasa leo siku ya tarehe 16 mwezi wa tatu jumatatu majira ya saa sita mjana mvua zimeanza kunyesha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na kuleta matumaini ya kupungua kwa joto kali lilokuwa limetawala.

Thursday, 12 March 2015



 UNGANA NA SURE HERBAL CLINIC KUPINGA MAUAJI YA ALBINO TANZANIA.